Wanafunzi wa chuo cha DAR ES SALAAM CITY COLLEGE wakijisomea wakati wa mitihani yao ya mwisho katika chuo hicho.
Wanafunzi wengi wa vyuo vya kati nchini Tanzania wenye malengo ya kufanikiwa katika maisha yao kutokana na elimu wanayoipata katika vyuo hivyo, wanahitaji kupewa kipaombele kutoka serikalini kwani vyuo hivyo vinatoa elimu inayowasaidia vijana wengi katika nchi yetu.
Vyuo hivyo vinavyotoa elimu ya cheti na Stashahada vimekuwa chachu ya kufaulisha wanafunzi wengi wanaojiunga na elimu ya juu nchini. Tofauti na elimu ya sekondari inayotolewa nchini ambayo imeonekana kusuasua katika miaka ya hivi karibuni , vyuo vya kati vimebaki kama nguzo na msingi imara wa elimu katika nchi yetu.
Aidha vyuo hivyo vimekuwa vikivumbua vipaji tofauti kwa vijana tofauti katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania, baadhi ya fani zanazotolwa katika vyuo hivyo ni Uandishi wa Habari ,Utawala, Ununuzi na Ugavi, Maendeleo ya Jamii pamoja na fani nyingine nyingi zinazoweza kuinua na kuendeleza maendeleo ya nchi yetu.
Baadhi ya vyuo vinavyotoa elimu ya cheti na Stashahada katika fani mbalimbali nchini ni pamoja na ROYAL COLLEGE OF TANZANIA, DAR ES SALAAM CITY COLLEGE, TIMES SCHOOL OF JOURNALISM, DATASTAR TRAINING COLLEGE vyote vya jijini Dar es salaam, ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE, NATIONAL COLLEGE OF TOURISM, Vya jijini Arusha.
Imetolewa na Deo Amon, ARUSHA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.