Ungana nami ujionee picha, habari mbalimbali kutoka hapa nchini na nje ya nchi pia.
Jumatatu, 11 Novemba 2013
GIZA NENE CHADEMA
Naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe
Katibu mkuu wa CHADEMA Willbroad Slaa
Mgogoro ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), umeingia katika sura mpya baada ya viongozi wake wawili waandamizi, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo kuuandikia uongozi wa chama hicho wakitaka uikane taarifa inayowachafua mitandaoni.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Zitto alisema amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa kumwomba athibitishe ‘Taarifa ya Siri ya Chadema’ kama ni ya kweli au chama hicho kiikanushe ili aweze kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waandishi wa kile alichokiita ‘hekaya.’
Taarifa ya Chadema inasema kwamba chama hicho kilikuwa kimechunguza mwenendo wa Zitto tangu mwaka 2008 hadi 2010 na kubaini kuwa Zitto anapokea fedha kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuivuruga Chadema,”
Zitto alisema taarifa hiyo ni ya kutunga na iliyojaa uongo wa kiwango cha kutisha, imemfedhehesha, imemsikitisha na kumkasirisha.
“Pengine lengo la ripoti hiyo lilikuwa ni kutaka kunipoteza kutoka katika nia na dhamira yangu ya dhati ya kutaka Watanzania wafaidike na utajiri wao. Muda ambao watunzi wa ripoti hiyo waliamua kutoa taarifa yao unazua maswali mengi kuliko majibu,” Alisema Zitto katika taarifa yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.