Nguli wa muziki wa jazz nchini Kenya, Joseph Hellon, ameuponda utaratibu mpya unaotumika kwenye shindano la Tusker Project Fame msimu wa sita wa kualika waongozaji wa muziki wapya kila wiki.
"Unawezaje kumchukua msanii wa rap awafundishe waimbaji? Namheshimu Muthoni the Drummer Queen lakini naamini angewatendea haki mashabiki zaidi ya kuongelea kuhusu ujasiriamali. Aliwafanya waimbaji warap na bado kwenye usahili unakuwa ‘disqualified’ kwa sababu hiyohiyo," alisema Hellon.
Amemponda pia Eric Wainaina ambaye ni principal kwenye academy kwa kusema:
Eric ni mtu anayeheshimika lakini anaonekana kupotea. Yupo hewani anaimba ‘happy birthday’ na kuigiza lafudhi. Anatakiwa kuonesha uwezo wake wa uongozi na kugawa maarifa yake. Sijaona maendeleo yoyote ya sauti na uwezo tangu washiriki wajiunge na academy."
Wiki iliyopita rapper wa Muthoni the Drummer Queen alikuwa muongozaji mkuu wa muziki kwa washiriki wa TPF6 na kabla ya hapo alikuwa Hermy B.
kwa habari kamili tembelea www.timesfm.co.tz
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.