MTOMTO AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA SHIMO LA CHOO
MBEYA,
Mwili wa Mtoto Joshua Isack (4) ukichukuliwa na polisi
Hili ndilo shimo alimokutwa marehemu Joshua
Tukio hilo la kuonekana kwa mtoto huyo
lilitokea jana majira ya saa Kumi jioni katika Mtaa wa Nyibuko Pambogo kata ya
Iyela Jijini Mbeya baada ya juhudi za wazazi na majirani kushirikiana kumtafuta
na kumpata akiwa amepoteza maisha ndani ya shimo la choo.
Akizungumza kwa uchungu na masikitiko
makubwa baba mzazi wa marehemu Isack Daniel ambaye ni mfanyakazi wa Mamlaka ya
Maji Mbeya alisema Mtoto wake huyo wa kiume alikuwa anacheza na wenzie jumatatu
ya Oktoba 28, majira ya saa 12 jioni lakini alitoweka katika mazingira ya
kutatanisha.
Alisema baada ya kuona giza linaingia na
mtoto hajarudi alianza kumtafuta katika kila eneo akishirikiana na baadhi ya
ndugu na majirani lakini hakufanikiwa kumwona kwa siku hiyo ambayo kesho yake
akiwa ni viongozi wa mtaa walienda kutoa taarifa kituo cha Polisi cha Kati
Mbeya Mjini.
Mzazi huyo aliendelea kusema baada ya
kutoa taarifa polisi bado waliendelea na juhudi za kumtafuta huku Ubalozi
ukiunda kikosi maalumu cha kufanya msako wa nyumba hadi nyumba ambapo baada ya
kupita katika nyumba ya jirani alipokutwa marehemu katika shimo la maji machafu
walipatwa na wasi wasi baada ya kuona kuna mabadiliko ya mbao zilizokuwa
zimefunika shimo hilo.
Alisema awali walivyopita siku moja
kabla waliona shimo hilo likiwa limefunikwa kwa mabanzi yaliyochakaa lakini
siku ya pili yake asubuhi walikuta kukiwa na mabanzi mapya kuashiria kuna
ukarabati umefanyika hali iliyowapa wasi wasi na kulazimika kulifunua shimo
hilo na kumkuta marehemu akiwa amepoteza maisha ndani ya shimo hilo.,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.