Mweusi Joh Makini toka Kaskazini, na Member wa Micharazo Mr. Blue ndio wasanii wa hip hop wa Bongo wanaofanya vizuri na wanaokubalika zaidi nchini Marekani japokuwa bado hawajapata mashavu ya kupiga shows pande hizo.
Hii ni kwa mujibu wa DMK, mmiliki wa Swahili radio na Swahili TV za Marekani ambaye pia ni promoter anaefanya kazi ya kuwapa deals za shows wasanii wa Afrika nchini Marekani.
DMK alifunguka kupitia ‘The Jump Off’ ya 100.5 Times fm.
“Kuna wanamuziki wazuri tu wa hip hop hapa ambao mimi nawakubali na watu wengi wanawakubali, lakini unajua nyakati zao kwa sasa hivi bado kidogo, kwa sababu unapowapeleka mwanamuziki kule lazima awe na ngoma ambazo zinaweza kuwatoa watu nyumbani na kuwapeleka kwenye show.” Alisema DMK.
“Kuna wimbo kama ule wa Mr. Blue ‘Pesa’, kuna mwingine wa Joh Makini ‘Bei ya Mkaa nini..wale wanakubalika sana kule. Kwa hiyo very soon usije ukashangaa kusikia Joh Makini ametua Marekani.” Aliaongeza DMK.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.