Ungana nami ujionee picha, habari mbalimbali kutoka hapa nchini na nje ya nchi pia.
Ijumaa, 15 Novemba 2013
DIAMOND KUTENGENEZA VIDEO NA CLARENCE NCHINI NIGERIA?
Diamond akiwa bado yuko nchini Nigeria ambako ameelekea kwaajili ya kumalizia collabo za wasanii wawili kati ya Davido na Iyanya,pamoja na kufanya video ya remix ya My Number One aliyomshirikisha Davido.
Sasa leo ameonekana akiwa na muongozaji wa videos Clarence Peters wa Nigeria ambaye ameshafanya video nyingi za mastaa mbalimbali wa hapa Afrika wakiwemo P Square.
Clarence Abiodun Peters ambaye ni CEO wa kampuni ya kutengeneza videos Capital Dreams,ameshawahi kuongoza video za mastaa wa hapa Afrika kama Bracket 'Me n You',P Square-Alingo,2 Face-Only Me na zinginezo.
Hii ndio picha aliyopost Diamond instagram na kuandika 'Last nyt, With Clarence Peters.... the Director of #Alingo #Personally Videos..... #Kokorikoooo'
Je Unadhani Clarence ndio director atakayefanya video ya Diamond Platinum?
Itazame hii video hapa uone Clarence Peters akitengeneza video ya Msanii 'Ice Prince' wa Nigeria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.