TEMBELEA

www.deoamon.blogspot.com

Jumatatu, 3 Februari 2014

JK AMPA SHAVU KINANA.








Mbeya.
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amemmwagia sifa Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana akisema amefanya kazi nzuri kwa kuwafikisha mawaziri wanne kwenye Kamati Kuu baada ya kubaini matatizo yanayohusu sekta zao.
Rais Kikwete alisema jana kuwa katika ziara ya viongozi wa Sekretarieti ya CCM mwishoni mwa mwaka jana, kwenye mikoa ya Ruvuma na Mbeya, Kinana alifanya kazi nzuri katika mazingira magumu kiasi cha kufikia kupanda meli kwenye Ziwa Nyasa.
Alisema akiwa kwenye ziara hiyo, Katibu Mkuu huyo aligundua matatizo kadhaa kwenye sekta za mawaziri husika na hivyo aliamua kuwafikisha Kamati Kuu ili watoe maelezo, jambo ambalo alisema linatakiwa kuigwa na viongozi wengine wa CCM.
“Najua wapo watu walitaka mawaziri hao wafukuzwe kazi. Kwa vile hilo halikufanyika, basi likageuzwa kuwa suala la malumbano. Napenda ieleweke kuwa kuitwa Kamati Kuu hakuna maana ya kuishia kufukuzwa,’’ alisema Kikwete. Alisema mawaziri hao waliitwa kwa sababu matatizo yaliyobainika yalitakiwa kupatiwa ufumbuzi na kwamba yalitolewa maelekezo kwa ajili ya utekelezaji.
Alisema Kamati Kuu inaendelea kufuatilia na kama hakutakuwa na maendeleo ndipo inapoweza kuomba mamlaka ya uteuzi ichukue hatua zinazotakiwa dhidi ya wahusika.
“Hongera Ndugu Kinana kwa kusimamia na kutekeleza kwa vitendo maazimio ya Mkutano Mkuu wa chama chetu,” alisema Kinana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.